Ama kweli haya ni maajabu makubwa ambayo watu wengi hawayafahamu, eneo hili linafahamika kama BERMUDA TRIANGLE jina lililopewa na Vincent H Caddis mwaka 1974,kutokana na maajabu yake eneo hilo pia huitwa DEVIL TRIANGLE ( Pembe tatu ya kishetani) eneo hili linapatikana katika bahari ya Atlantiki pia ni eneo linalotenganisha maeneo matatu kwanza kisiwa cha Bermuda, mji wa Miami Florida na nchi ya puertorico, eneo hilo lina ukubwa wa maili 500000

Maajabu makubwa ambayo tutayaongelea, KWANZA ni kupotea kwa ndege nyingi ambazo zimepita katika anga la eneo hilo PILI ni kupotea kwa meli nyingi zinazopita katika eneo hilo. na kubwa zaidi ni kutopatikana kwa taarifa yoyote kuhusu mahali ambapo meli na ndege hizo huelekea baada ya kupotea. Swali kubwa linalozuka ni Je ninini chanzo kikubwa cha kupotea kwa vyombo hivyo? kwa miaka mingi iliyopita chanzo chake hakikujulikana, lakini katika uchunguzi uliofanywa hivi karibuni na kituo kikubwa ulimwenguni cha uchunguzi wa anga NASA, inahisiwa kuwa eneo hilo limezungukwa na nguvu za usumaku zinazofanya kutokea kwa nguvu kubwa ya uvutano inayovuta kitu chochote kinachopatikana eneo hilo au katika anga la eneo hilo

Pia inahisiwa kuwa katika eneo hilo kuna kemikali ya METHANE iliyoyeyuka na kuchangamana na maji hayo jambo linalofanya maji ya eneo hilo kutokuwa na uwezo wa kuhimili uzito wa meli katika eneo hilo, swali ni je kuna uhusiano gani kati ya upotevu wa ndege na uwepo wa kemikali katika maji? katika kumbukumbu zilizopo mwaka 1948 ndege aina ya NC16002 iliyopakia abiria watatu ilipotea katika eneo hilo ilipokuwa ikitoka puertoerico kuelekea miami, Frorida nchini Marekani pia miaka mitatu nyuma mwaka wa 1945 ndege 5 za kijeshi za Mrekani zilipotea katika eneo hilo. hicho ndicho kilichochochea uchunguzi mkubwa kufanywa ili kutambua sababu za vyombo hivyo kupotea katika eneo hilo. NAKUSHUKURU SANA MTU WANGU KWA KUTEMBELEA BLOG HII NA KUSOMA HABARI HII Ili kupata habari nyingine nyingi zilizochunguzwa kikamilifu endelea kutembelea blog hii kila unapopata fursa.
Post A Comment:
0 comments:
Chapisha Maoni