Hii ni sayari mpya iliyogunduliwa na wanasayansi inayofanana kabisa kitabia na dunia, sayari hii inaitwa KEPLER 186F ipo katika mzunguko wa kipekee sana unaoitwa kepler186 system, mzunguko huu ni tofauti kabisa na huu wakwetu tuliopo wa solar system, kwani mzunguko wa kepler haulizunguki jua hili tunalolifahamu, wenyewe una jua lake la tofauti TAZAMA PICHA HAPA CHII
Hilo ndilo jua linalozungukwa na sayari hiyo linaitwa RED DWARF, sayari hiyo ina maji pia ina joto linaloweza kufanya viumbe hai kuishi, kwa ukubwa sayari ya kepler 186f ni kubwa kidogo kwa Dunia ukubwa wake ni mara 1.75 zaidi ya dunia , sayari hiyo hulizunguka jua kwa siku 130, hivyo hulizunguka jua lake kwa siku chache kulinganisha na Dunia ambayo ni siku 365. sayari ya kepler ipo umbali wa maili milioni 32.5 sawa na kilomita milioni 52.4 kutoka katika jua TAZAMA PICHA HAPA CHINI


Post A Comment:
0 comments:
Chapisha Maoni